

Injili hii inaanza kwa kuorodhesha mababu wa Yesu. Mathayo anakazia pia mafundisho ya Yesu ilhali Marko anaeleza zaidi matendo yake.


Tabia hii inachukuliwa kuthibitisha maelezo ya kwamba Injili hii ililenga Wakristo ambao walikuwa Wayahudi na kutumia lugha ya Kigiriki. Kwa sababu hiyo Mathayo anaripoti maneno ya Agano la Kale mara kwa mara ili kuthibitishwa yametimia katika maisha ya Yesu. Mathayo anakazia kuwa Yesu wa Nazareti ndiye Masiya aliyetangazwa na ma nabii wa Agano la Kale. Wakati wa kutolewa unaaminiwa na wataalamu wengi wa kisasa ilikuwa kati ya mwaka 80 na 90, yaani baada ya hekalu la Yerusalemu kubomolewa, tena baada ya Wayahudi kuwatenga wenzao waliomuamini Yesu. Wataalamu wanajadili kiasi gani maandishi yake yamechangia Injili hii jinsi ilivyo. Ingawa Injili yenyewe haimtaji mwandishi wake, kuanzia Papias (mnamo mwaka 130) Mtume Mathayo ametajwa kama mwandishi wa misemo ya Yesu Kristo kwa lugha ya Kiebrania. Katika matoleo ya Biblia kichwa cha kitabu ni "Injili kama ilivyoandikwa na Mathayo" lakini kichwa hiki si sehemu ya toleo asili la Kigiriki. Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu. Huhesabiwa kati ya Injili Ndugu pamoja na Marko na Luka, kwa sababu inafanana nazo kwa kiasi kikubwa hasa inatumia asilimia 80 ya maandiko ya mwinjili Marko. Injili ya Mathayo ni kitabu cha kwanza katika orodha ya vitabu vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Mchoro huu kutoka Ufaransa (mnamo mwaka 800) wamuonyesha Mwinjili Mathayo akipokea maneno ya Injili yake kutoka kwa malaika.
